Jumanne , 9th Feb , 2016

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman amesema kuwa mahakama itatumia fedha walizopewa na serikali jumla ya shillingi billioni 12.3 kuboresha majengo ya mahakama ikiwa ni pamoja kuboresha makahama pamoja na kujenga mahakama za mwanzo

, wilaya na mahakama za hakimu mkazi ili kuwezesha kusikilizwa kwa mashauri mapema.

Akiwa ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Harrison Mwakyembe katika mahakama ya rufaa jijini Dar es salaam leo, Jaji Mkuu amefafanua pia kuwa fedha hizo zitasaidia kurejesha mahakama zilizokuwa zimefungwa kutokana na kukosekana pesa za kuziendesha..

Akielezea kuhusu matumaini ya wizara ya fedha kuhusu kutolewa kwa fedha Dk. Philip Mpango amesema kuwa bado wanaamini kuwa mahakama ikiwezeshwa katika kutoa haki itasaidia fedha zaidi kupatikana kama ilivyokuwa imani ya rais.