Rais Magufuli akifanya Mazungumzo na Rais Kagame wa Rwanda(picha na Maktaba).
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa imesema kuwa katika ziara hiyo wanatarajia kufungua miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Rais Dkt. John Magufuli akiwa nchini Rwanda akiwa pamoja na Mwenyeji wake rais wa nchi hiyo Paul Kagame wanatarajia kufungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha Mpakani.
Miundombinu hiyo iliyopo mpaka mwa Tanzania na Rwanda inafungua milango kwa nchi za Afrika Mashariki na katika na Ukanda wa bahari ya Hindi lakini pia ikiwa ni kukuza uhusiano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baada ya Uzinduzi huo viongozi hao wawili watakwenda Jijini Kigali ambako watakuwa na mazungumzo muhimu pamoja na kuweka shada la maua ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini humo.