Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
Jopo hilo la watu mashuhuri linaongozwa na wenyeviti wenza ambao ni Rais wa Chile Mhe. Michelle Bachelet na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn, huku Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Finland Mhe. Tarja Halonen wakiteuliwa kuwa wenyeviti mbadala.
Katika Pongezi hizo Rais Magufuli amesema kuteuliwa kwa Rais Kikwete kuwa miongoni mwa jopo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumeijengea heshima Tanzania na kumechochea matumaini ya mafanikio ya kukabiliana na changamoto za afya ya mama na mtoto hususani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ambayo jopo hilo litamshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwemo katika kuimarisha afya ya uzazi wa mama na mtoto.