Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na kulia ni Martha Umbula wakati wa uhai wake
Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 21, 2021, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kwamba Rais Magufuli, anakumbuka jitihada zake za uongozi akiwa mkuu wa wilaya na mbunge na kuwaomba wanafamilia wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Kifo cha Martha Umbula, kimetokea usiku wa kuamkia leo kilichotokea nchini India, katika Hospitali ya HCG Mumbai, alipokuwa anatibiwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaratibu mipango ya mazishi