Jumanne , 17th Mei , 2022

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, amesema kwamba katika kupunguza matumizi ya fedha za serikali kwenye suala la mafuta ni vyema magari ya viongozi wanaposhuka kwenda kwenye vikao yawe yanazimwa na madereva kushuka chini.

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson

Kuali hiyo ameitoa hii leo Mei 17, 2022, bungeni jijini Dodoma, na kusema haiwezekana kiongozi hayupo ndani ya gari lakini gari linaendelea kuwaka likingoja yeye arudi na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.

"Matumizi ya pesa kwenye eneo la mafuta yanakuwa makubwa sana kwa sababu ya magari kuendelea kuwaka wakati kiongozi hayupo kwenye gari , ameshuka ana mkutano wa saa mbili gari inaendelea kuwaka, Mhe. Waziri Mkuu uko hapa tunatamani tuone mabadiliko ili matumizi ya serikali kwenye eneo la mafuta yapungue," amesema Dkt. Tulia