Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma,
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Naliendele wa kuwapongeza wapiga kura wake kwa kumchagua, amesema hatua hiyo inatokana na ahadi iliyotolewa na serikali kupitia bodi ya TANESCO ambapo iliahidi kumaliza kero ya kukosa miundombinu ya umeme kwa maeneo yaliyobaki katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Amesema, kupitia kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ambaye yeye ni mjumbe, ilishawahi kuwaita viongozi wa TANESCO na kuwauliza maswali kadhaa ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kwanini maeneo yaliyopo ndani ya manispaa ya Mtwara hayana umeme wakati mitambo ya kuzalisha huduma hiyo ipo ndani ya manispaa hiyo.
Mbunge amesema kuwa mpaka kufikia mwezi Julai mwaka huu, wakiwa bado hawajapatiwa umeme basi zitatumika nguvu za umma kwa kufanya maandamano kudai huduma hiyo.