Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam Awadhi Haji amesema zoezi maalumu lakukamata abiria na waendesha bodaboda ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani zakuvaa kofia ngumu limekua na changamoto kubwa yakukosa ushirikiano kutoka kwa madereva hao.
Ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio nakuongeza kuwa zoezi hilo limewashirikisha wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakiwemo mamlaka ya uthibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA ambao ukaguzi huo umebaini makosa mbalimbali ikiwemo kosa la madereva wengi kutokua na vibali vya kuendesha vyombo hivyo vya moto na wanamakosa ambayo yanawafanya washindwe kutii sheria bila shuluti.
Amesema kwa mujibu wa sheria za miji zakuzuia bodaboda kuingia katikati ya miji zimekua zikivunjwa kutokana na madereva hao kukosa uelewa wa sheria mbalimbali za barabarani zinavyoelekeza.
Adha ameongeza kuwa maderava bodaboda wamekua wakisababisha ajali mbaya ambazo zingine husababisha vilema vya maisha na zingine kuwasababishia kupoteza maisha kabisa hivyo wameamua kufabya zoezi hilo kikamilifu kwakuwakamata na abiria pia ambao hawavai kofia ngumu ili kuepusha upotevu wa nguvu kazi ya taifa usiendelee kutokea.






