Jumatatu , 4th Mei , 2015

Umoja wa Madereva nchini Tanzania leo wametangaza mgomo wa nchi nzima kwa vyombo vyote vya mto vya usafirishaji kutokana na ukimya dhidi ya madai yao kwa serikali kwa walivyokubaliana katika kikoa cha tarehe 10 April mwaka huu.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Ktibu wa umoja wa Madreva na Chama cha Malori, Bw. Rashid Salehe amesema mgomo huo upo palepale kwa madai kuwa bado kuna mambo ambayo yameendelea kuwa kikwazo kwao.

Katika mkutano mkuu waliofanya jijini Dar es Salaam Salehe amesema kuwa moja kati ya madai yao makuu ni pamoja na kutaka kupewa ajira rasmi na waajiri wao, posho za safari na masomo, kufuta kusoma kila baada ya leseni kuisha, pamoja na bima.

Kwa upande wake katibu wa chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania TABOA, Ernea Mrutu amesema walipata taarifa ya mgomo huo na kueleza kwamba wanaotangaza mgomo sio madereva walioajiriwa.

Naye mwenyekiti wa wamiliki wa daladala Dar es Salaam (DARCOBOA), Sabri Mbarouk amesema chama hicho kina taarifa ya mgomo huo lakini akaeleza kusikitishwa kwake kwa namna ya madereva wa vyombo vya usafiri wanavyowahusisha huku akisema wao hawahusiki na hilo.

Awali jana usiku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick na Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Suleiman Kova walitawaataka madereva hao wasigome na badala yake viongozi wao watakutana na waziri mkuu Mizengo Pinda kwa ajili ya kufanya mazungumo.