Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 07 Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).
Dkt. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu tarehe 30 Juni, 2016

