
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo
Akiongea kupitia kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, Oliver amesema mwanzo alikuwa anaripoti tu taarifa za Mazingira lakini sasa atakwenda mbali zaidi kwa kuhusika moja kwa moja kuhamasisha usafi wa mazingira kwa jamii.
''Baada ya uteuzi huu najiona sasa nina jukumu kubwa la kusimamia usafi wa mazingira ikiwemo kutoa elimu lakini pia hata kumfuata mtu mmoja mmoja ninapoona amefanya kitu cha tofauti juu ya kutunza mazingira ikiwemo kutupa taka eneo ambalo sio sahihi,'' amesema Oliver.
Soma taarifa kamili ya uteuzi