Jumanne , 10th Mei , 2016

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku Galawa, amewaagiza Maafisa Tarafa kushiriki katika zoezi la uhakiki wa watumishi katika halmashauri za mkoani humo ili kuwezesha shughuli hiyo kuwa na tija zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa.

Katika kikao chake na maafisa hao,Galawa amewaagiza maafisa hao kuwa na majina na idadi ya watumishi wote waliopo katika maeneo yao ili kuwezesha utunzaji mzuri wa rekodi za watumishi.

Wakati huo huo Galawa ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kuleta orodha ya watumishi wote wakiwamo waliopo masomoni ambapo taarifa zao zinapaswa kuonesha walianza lini masomo na wanataraji kumaliza lini.

Amesema taarifa hizo zitaiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za watumishi waliopo sambamba na sifa za kitaaluma sambamba na mapungufu yaliyopo katika kada tofauti za utumishi wa umma.