Jumamosi , 2nd Jul , 2016

Serikali ya Kenya imesema kwamba itawafungulia mashitaka ya mauaji maafisa watatu wa polisi kufuatia ugunduzi wa vifo viwili.

Mahakama kuu ya Kenya.

Mwili wa wakili wa haki za binadamu Willie Kimani na dereva wa taxi ilipatikana ikielea katika mto, kaskazini mashariki mwa Nairobi hapo jana Ijumaa.

Vifo vyao vinaaminika kuhusiana na kesi iliyoko mahakamani ambayo wakili Kimani alikua akimtetea mwanaume mmoja Josephat Mwenda, anayeilamu polisi kwa mateso.

Mamlaka zinashuku kwamba maafisa hao wa polisi wamehusika na utekaji nyara, mateso na mauaji ya wanaume hao watatu.
Rais wa chama cha mawakili nchini Kenya amesema mawakili wote nchini humo watafanya mgomo wa nchi nzima kulaani mauaji hayo.