Aliyekuwa Mkuu wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki ambae sasa amehamishiwa Mkoani Kilimanjaro.
Said Mecky Sadiki ambae amehamishiwa Mkoani Kilimanjaro ameyasema hayo jana wakati akipokea vifaa vya Ujenzi wa vyumba vya madarasa vyenye thamani ya shilingi milioni 200 kutoka katika makampuni ya MM1 STEEL na Export Trading.
Akipokea msaada huo Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa msaada huo utaboresha utoaji wa elimu ya msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuahidi atawaachia wasimamizi wa wilaya wakiwemo Ma-DC ili vifaa hivyo viweze kuwafikia walengwa moja kwa moja.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema, amesema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ongezeko la wakazi linalozidi idadi ya shule huku Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi, akitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuchangia sekta ya elimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya MMI STEEL,Stubash Patel amesema wameguswa na suala la elimu kwa kuwa ndio kitu cha msingi katika maisha ya mwanadamu katika kujitafutia riziki ya kila siku.