
M23 inashikilia eneo kubwa zaidi kuliko hapo awali mashariki mwa Congo baada ya kufanya harakati za mapema mwaka huu.
Mapigano hayo yamewaua maelfu ya watu na kuwafanya mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo hayo, waziri wa Mambo ya nje wa DRC Therese Kayikwamba Wagner amesema haya ni mazungumzo ambayo yalifanyika ndani ya mfumo wa mchakato wa Doha na ambayo lazima yaendelee ndani ya mfumo wa mchakato wa Doha. #EastAfricaTV