Jumatano , 6th Dec , 2017

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema kwamba hawezi kuhama CHADEMA na kwenda CCM wakati yeye alishughulika kuwashawishi baadhi ya watu kuhamia katika chama alichopo sasa hivi.

Kubenea amesema kwamba ana mchango mkubwa sana katika kumuingiza Lowassa pamoja na Sumaye CHADEMA hivyo angejiona  mwendawazimu kuwasaliti watu ambao walimuamini na kwenda kwenye Chama ambacho yeye aliwaondoa.

"Mimi ningetaka kuondoka CHADEMA, ningeondoka kwa dhamira yangu mwenyewe lakini siyo kwa kushawishiwa au kwa kufika bei. Bei yangu ni utu wangu. Mimi sina bei kabisa hata kama Ingetengwa bajeti nzima ya serikali isingeweza kuninunua. Kiufupi sina bei.  Nimejenga jina kwa miaka 15 pamoja na sifa nzuri za chama changu nili struggle kwa kupata nafasi ya kutunga sheria siwezi kuwasaliti watu wa ubungo na hata wale walionichangia sumni sumni" Kubenea.

Mh. Kubenea

Ameongeza kwamba "Naendaje CCM, wakati huo huo mimi nilishiriki kuwavuta CHADEMA Mawaziri Wakuu wawili Lowassa na Sumaye. Sasa kweli nawezaje kuhama chama na kuwaacha hao watu na wengine wengi tu kwa ajili ya kuhamia CCM nitakuwa sina akili. Uweli nimeumizwa na huo uzushi.

Mbali hayo Kubenea ameongeza kwamba  anashangaa Chama hicho kinachoitwa cha wanyonge (CCM) kimefukuza wafanyakazi wengi wanaodaiwa kutokuwa na vyeti lakini watu waliofukuzwa walitumikia nchi kwa miaka mingi na wamefukuzwa kazi bila hata kifuta jasho huku kukiwa na mtu ambaye anatumia jina lisilo lake na chama chake kinamkumbatia.

Amefafanua kuwa wakati mwingi alikuwa akitumia nafasoi na tashi wake katika kukosoa hivyo hajaona jipya ambalo CCM wanaweza kufanya kwani hata hicho kinachoitwa kupambana na rushwa wameshindwa na badala yake kimempandisha cheo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na kuwa Mkuu wa Mkoa licha ya kutuhumiwa kwa rushwa na ushahidi ulionyesha

Pamoja na hayo kubenea ameweka wazi kwamba "Hakuna jambo ndani ya chamba changu ambacho kinaweza kunishawishi mimi kukihama