Jumamosi , 1st Aug , 2015

Mh. Edward Lowassa amerejesha fomu ya kugombea urais CHADEMA na mwenyeji wake Makamu Mwenyekiti bara wa CHADEMA Prof Abdallah Safari amepokea fomu hizo.

Prof Safari amesema mpaka sasa hakuna mgombea yoyote wa Chadema zaidi ya Mheshimiwa Edward Lowassa aliyechukua fomu ya kugombea Urais.

Mheshimiwa Edward Lowassa amedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni 1 na laki 6.