
Moja ya daladala iliyogongwa na lori Arusha
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kusema kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini sababu ya lori hilo kupoteza mwelekeo na kusababisha maafa hayo.
Aidha Kama Masejo amesema kuwa, majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru, mkoani humo.