Mkuu wa Wilaya ya Longido Ernest Kahindi
wakiongea na kituo hiki baadhi ya wakazi wa eneo hilo amesema kuwa, jamii hiyo ya wafugaji imekuwa haina utamaduni wa kuwa na vyoo katika kaya nyingi hivyo kujisaidia vichakani hali ambayo inaweza kuhatarisha afya za wakazi hao kutokana na ugonjwa wa kipindupindu ambao bado haujabisha hodi katika mji huo.
Mkuu wa wilaya ya Longido Ernest Kahindi amesema kuwa wameanza kuhamasisha ujengaji wa vyoo katika familia za jamii hiyo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa upande wao viongozi wa Longido Team Mazingira ambayo awali ilikuwa 'Team Magufuli' na kubadilika ili kuunga mkono adhma ya Rais Magufuli kulinda mazingira, mwenyekiti wa wilaya hiyo Atanas Kijuu na katibu wake Nai Israel wamesema licha ya tahadhari hiyo ya ugonjwa wa kipindupindu, wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uchomaji mkaa ambazo husababisha ukame na vyanzo vya maji kuharibika.
Ili kunusuru mazingira na shughuli za uchomaji mkaa Longido timu Mazingira ina mpango ya kuanzisha Saccos itakayoanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji kuku ili kuanzisha shughuli mbadala za kiuchumi tofauti na uchomaji mkaa.