Jumamosi , 4th Jul , 2020

Mwenyekiti  wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, kwa kutumia mamlaka ya kikatiba ya chama hicho, amemsimamisha Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Faki Suleiman Khatib.

Prof. Ibrahim Lipumba

Hatua hiyo imefikia ikiwa ni katika utekelezaji wa agizo la Baraza Kuu la kuondoa mapungufu na kuimarisha Kamati Tendaji ya chama hicho.

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar itajazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linalotarajiwa kuketi mwishoni mwa mwezi huu.

Mwenyekiti amemteua Nadhira Ali Haji kuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Katibu Mkuu wa chama, Haroub Mohammed Shamis.

Mwenyekiti ameyafanya hayo mapema leo huko Zanzibar kwenye ziara fupi ya kumtambulisha Katibu Mkuu mpya na kushughulikia maagizo aliyopewa na Baraza Kuu lililoketi wiki iliyopita ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo, Jijini Dar es Salaam.