Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla
RC Makalla ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa Masoko Wilaya ya Temeke ambapo amesema changamoto za masoko lazima zipatiwe majibu hususani suala la daladala kutokupita katika maeno ya masoko.
“Nimekuja na Mkuu wa Wilaya yeye ndio Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama, LATRA wapo tunataka mabasi yaje hapa DC Simamia, LATRA waite na mimi naagiza ndani ya wiki moja nitakuja nataka kukuta daladala hapa, tusibembelezane dalala zije hapa shida nini watu wakishuka hapa watanunua kitu cha kwanza, watatamani na kitu kingine,” amesema RC Makalla.
Pia RC Makalla ameeleza kuwa baadhi ya watendaji ndio wanakwamisha masoko kutokana na kutokuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo masokoni, huku akisema kuwa baadhi ya ubunifu kwenye masoko hauzingatii utamaduni wakitanzania.
