Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 6, 2021, wakati akizindua kiwanda cha Elsewedy Electronic East Africa Limited kilichopo Kisarawe II, Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
"Unaambiwa ukiwa kiongozi una maswali ya kujibu kwa Mungu, na mimi ndiko ninapopaogopa zaidi, nafanya ninavyoweza ili nikifika huko kesho na keshokutwa nikiulizwa niseme nimefanya hiki, kwa usafi, kuliko kwamba ooh nilisema sikusikilizwa, nataka nijisafishie njia yangu," amesema Rais Samia.