Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya
Kusaya ametoa agizo hilo leo Oktoba 20 akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa ya kukagua utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo pamoja na kutatua changamoto za kiutendaji.
" Natoa agizo kwa wakandarasi wanaojenga miradi ya ujenzi wa vihenge vya kisasa na maghala kwa ajili ya kuongeza uwezo wa NFRA kuhifadhi nafaka kuwa wakamilishe kazi ifikapo Desemba 2020. Sitoongeza muda kwa mkandarasi yeyote,"amesema Gerald KusayaKatika hatua nyingine Kusaya ametoa onyo kali kwa kampuni ya Feerum ya Poland inayochelewesha kukamilisha mradi wa vihenge Songwe kwa kisingizio cha virusi vya corona na kusema kuwa endapo hatakabidhi kazi ifikapo Desemba taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mkataba wake.