Naibu Waziri Masauni ametoa kauli hiyo visiwani Zanzibar, wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani, juu ya hali ya usalama wa maeneo mbalimbali hususani kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.
"Kuna watu hawana nia njema na Serikali hasa kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi, na katika kufanya hivyo wanatafuta mianya ya kupenyea, sisi tumepewa dhamana katika maeneo mbalimbali si vizuri tukaweka mianya hiyo, kwa sababu tunafanya kazi kwenye Sertikali ambayo inatakiwa kuchafuliwa." amesema Masauni
"Tukitaka kuanzia sisi lazima tuondoe mianya yote ambayo, ya watu wasiokuwa na nia njema ya Serikali na wananchi wake ili wasiichafue." ameongeza Masauni
Hivi karibuni akiwa visiwani humo Naibu Waziri Masauni aliitaka Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, kuhakikisha inatoa huduma iliyobora kwa Watanzania.

