
Mpango ameyasema hayo alipowasilisha Bungeni bajeti ya serikali ya trilioni 29. 5 ambayo imevuka bajeti ya mwaka jana kwa trilioni 7 ambapo bajeti ya maendeleo kwa mara ya kwanza ni asilimia 40 ya bajeti yote tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilifikia asilimia 25%.
''Kuanzia tarehe 1/07/2016 ni marufuku kwa taasisi na idara za serikali kufanya biashara na mtu asiyetumia EFDs '' amesema Waziri Mpango.
Aidha Wafanyabiashara wametakiwa kutumia mashine za kutoa risiti wanapouza bidhaa tofauti na hapo watanyang'anywa leseni za biashara walizopewa na Mamlaka ya Mapato Nchini TRA.
Aidha serikali imetenga shilingi bilioni 44.7 kwa ajili ya kuiwezesha Ofisi ya Ukaguzi wa fedha za umma CAG ili kuwezesha taasisi hiyo kuweza kukagua ofisi za umma na kuhakikisha fedha za serikali zinatumika kama ilivyokusudiwa.