Vifaa vya kivita vya jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ.
Akizungumza jijini Dar es salaam mkuu wa jeshi la nchi kavu Meja Jenerali Salim Kijuu amesema kongamano hilo litakua sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi(JWTZ).
Ameongeza wajumbe toka nchi za SADC,Umoja wa afrika na jumuiya nyingine za kimataifa watakutana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha ulinzi na usalama duniani kwa sasa na siku za usoni.
Kwa mujibu wa Meja Jenerali Kijuu, kongamano hilo litahusisha pia maonyesho ya zana za kivita ambapo makampuni zaidi ya 32 kutoka ndani na nje ya bara la Afrika yataonyesha zana mbali mbali za kivita.





