Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto, mkoani Tanga katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Soni wakati akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli na wagombea udiwani baada ya mgombea ubunge wa jimbo hilo January Makamba kupita bila ya kupingwa.
"Najua msimu huu mmehangaika sana, lazima kiwanda chetu kianze kazi na hatua zote za msingi zimeshakamilika, msimamizi mkuu ni Msajili wa Hazina na mwekezaji ni mifuko ya hifadhi ya jamiii ya PSSSF na WCF, ambao walishakuja kufanya ukaguzi ila kuna mitambo inahitaji vipuri na tumeagiza vichongwe ili kazi ianze chai isindikwe", amesema Kassim Majaliwa.
Kiwanda cha chai cha Mponde ni miongoni mwa viwanda vya kusindika majani mabichi ya chai katika Halmashauri ya Bumbuli na hutegemewa na wakulima wadogo wa chai wapatao 5,000 kama soko la majani mabichi ya chai kutoka katika mashamba yao, ambapo uzalishaji ulisimama kufuatia mgogoro uliojitokeza mwaka 2013.