Jumanne , 18th Aug , 2015

Watu wawili wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jiji la Dar es salaam na wengine 30 wamelazwa katika hospitali katika za wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid

Akiongea na East Africa Radio Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty amesema ugonjwa ulianza siku ya Jumamosi baada ya mtu mooja kufariki kwa kuhara na kutapika na baadaye kubainika watu wengine wanne.

Natty amesema kuwa mpaka sasa wagonjwa karibu ya thelathini wamewekwa karantini huku wanne kati ya hao wakiwa wamethibitika kuumwa ugonjwa huo na wengine 19 wakiwa wamelazwa katika hosptali ya Sinza.

Natty amesema manispaa ya Kindoni imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka karantini katika maeneo ambayo ugonjwa huo upo huku akiwataka wananchi kuchukua hatua mbalimbali za kutumia maji safi na salama kwa kunywa pamoja na kula chakula katika mazingira uya usafi.