Zaidi ya shilingi bilioni 13 zinatarajiwa kukusanywa na halmashauri ya manispa ya Kinondoni ikiwa ni kodi ya mabango madogo na makubwa yanayoonekana maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.
Akibainisha hayo meya wa manispaa ya Kinondoni amesema kuwa katika kipindi hiki manispaa imedhamiria kutumia fursa za mapato yake kwa asilimia 100 hivyo wameamua kufanya mapitio upya ya walipa kodi wake hasa kwenye ushuru wa huduma, kodi ya majengo, leseni za biashara na vileo, ushuru wa nyumba za kulala wageni na uwekezaji.
Aidha manispaa inawataka wamiliki wote wa mabango kulipa fedha hizo za ushuru ndani ya siku saba kwani baada ya muda huo mabango yote yataondolewa na mhusika atachukuliwa hatua za kisheria.



