Jumanne , 22nd Jul , 2014

Rais Jakaya Kikwete ameipongeza halamshauri ya wilaya ya Songea vijijini kwa kusimamia mradi wa maendeleo ukiwemo wa ujenzi wa soko la kimataifa lililojengwa mpakani kwa Tanzania na Msumbiji litakalowezesha kuongeza uchumi wa nchi.

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete amewataka wafanyabiashara kwa sasa kulitumia soko hilo ambalo limejengwa ka gharama ya serikali kwa biashara zote kati ya Msumbiiji na Tanzania ni vyema zikapitia katika soko hilo ili kuleta maendeleo kwenye vijiji jirani.

Amewataka wafanyabiashara wa mkoa wa ruvuma wasibweteke na biashara walizonazo na badala yake waangalie mbali kwa kutafuta biashara nchi jirani kupata soko la kimataifa.

Wakati huo huo, zaidi wa watu milioni 1.2 ambao ni masikini na wanaoishi kwenye hali duni wanatarajia kunufaika na mpango wa tatu wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF).

Akizungumza mkoani kilimanjaro mwakilishi wa mkurugenzi wa mpango huo taifa Ladislaus Mwamanga amesema mapango huo unatarajia kutilia mkazo sekta ya Elimu, Afya, na Lishe.

Fedha ni pamoja na mkopo wa bank ya dunia wa sh bilioni 330 huku serikali ya Tanzania ikichangia sh bilioni 45 wakati nchi hisani, Uingereza imetoa sh bilioni 24, Uhispania sh.Bilioni 9 na Marekani ni sh bilioni 1.4