Salva Kiir
Uteuzi huyo wa Machar uliotangazwa na televisheni ya taifa unachukuliwa kuwa ni sehemu ya makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza machafuko yaliyodumu kwa muda wa miaka miwili.
Sudani Kusini imekuwa katika machafuko tangu Desemba 2013, wakati mapigano yalipoibuka baina ya vikosi vitiifu kwa Kiir na wanajeshi wanaomuunga mkono Riek Machar, ambaye awali alikuwa makamu wa Rais.







