Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Kigwangalla anatumika vibaya" - Nyalandu

Jumatatu , 13th Nov , 2017

Aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amefunguka na kudai kuwa  Waziri wa sasa wizara hiyo Dkt. Hamisi Kigwangalla anatumika vibaya katika kumchafua na kueneza uzushi juu ya utumishi wake.

Nyalandu amefunguka hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook na kusema kwamba anasikitika kuona waziri huyo ametumia muda wake ndani ya bunge kumchafua, kumdhihaki pamoja na kusema uongo dhidi yake ikiwa anatambua kwamba ni njama za makusudi zilizopangwa kumchafua baada ya kuhama ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha Mh. Nyalandu amefunguka kwamba kinachofanywa juu yake ni  hatua ambayo imepangwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayethubutu ama kudiriki tena kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM katika Serikali ya awamu ya tano.

Nyalandu ameongeza kwamba Waziri "Kigwangalla anatumika vibaya, kwa u za uongo na uzushi aliuanza dhidi yangu mara tu alipoteuliwa, kwa kuanza kutoa kauli za kejeli dhidi ya utumishi wangu uliotukuka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na wenye rekodi thabiti" - Nyalandu.

Ameongeza "Propaganda za Kigwangalla ameamua zimuhusu Waziri moja tu wa Maliasili, Lazaro Nyalandu, jambo linalothibitisha njama na Progaganda za kuzimisha moto na nguvu ya umma kupitia upinzani, hasa baada ya kitendo changu cha kukihama CCM".

Kati ya habari ambazo Mh. Nyalandu amedai kuwa ni za uzushi ni pamoja na Dkt Kigwangalla kusema bungeni kwamba kiongozi huyo alikuwa akitumia helikopta kugombea urais 2015 kitu ambacho Nyalandu amekipinga na kufafanua.

"Mwaka 2015 nilitumia Helicopter kwa siku tatu za kumalizia Kampeni, na nilikodi helikopta hiyo kwa Sh milioni tano kwa siku (Jumla, milioni 15). Pia ingependeza kama hamaki za Kigwangalla zingemkumbusha kuwa Waziri Nyalandu akiwa Wizarani alipatia Serikali Helikopta mpya Moja, alileta ndege kwa matumizi ya kupambana na Ujangili. Alishawishi benki ya dunia, Ujerumani na USA kuleta mamilioni ya dola za kmarekani kusaidia mapambano hayo, na kwamba alifanikiwa sana kutokomeza ujangili nchini. Rais Kikwete alikiri hili wakati wa kuzindua Tangazo la Tanzania (Tanzania, the soul of Africa)," Nyalandu.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali