Alhamisi , 12th Mar , 2020

Wabunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, Ester Matiko na Ester Bulaya, wanatarajiwa kuzungumza leo mbele ya Vyombo vya Habari mara tu watakapotoka gerezani, baada ya faini zao kulipwa siku ya jana.

Wabunge Ester Matiko, Ester Bulaya na Halima Mdee.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Machi 12, 2020, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameendelea kuwashukuru wananchi walio ndani na hata nje ya nchi kwa kujitoa kwao na kwamba Wabunge hao ambao tayari wamekwishalipiwa faini zao watakuwa na jambo la kuzungumza baadaye.

"Kina Halima na wenzake watatoka asubuhi hii na baadaye watakuwa na mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya chama na sasa tunaendelea kuwahimiza wananchi kuendelea kuchangia ili tuweze kuwanusuru viongozi wengine waliobaki" amesema Mbowe.

Jana zilitumika Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kuwalipia faini zao wabunge hao na kuwanusuru na kifungo cha miezi mitano jela.