
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Dkt Kikwete ametoa kauli hiyo hii leo Julai 24, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa salamu za pole kwa Watanzania na kuwataka wawe na moyo wa subira na ustahamilivu wakati wa kipindi cha maombelezo ya kifo cha Rais Mkapa.
"Kifo ni siri ya Mwenyezi Mungu jana jioni nilikwenda kumuona hospitali, tukazungumza sana, alikuwa na maumivu lakini si maumivu ambayo ukitoka unakuja kuwaambia wenzake eeh huyu mgonjwa, nilivyopata taarifa usiku kama amefariki nikauliza kimetokea nini tena, na nimeondoka nikimuaga kwamba nitakuja tena kesho kukuona , kifo ni siri kubwa maana yake ungekuwa unajua ungeweza kusema hata tunaagana kabisa", amesema Dkt Kikwete.