Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo, Thomas John amesema kwamba wananchi walikibaini kichanga hicho baada ya kuburuzwa na mbwa kutoka kichakani kilikokuwa kimetupwa.
“Mtoto mchanga naona amezaliwa alfajiri ya leo (jana) na kutelekezwa na mama yake ambaye hadi muda huu wa saa 11 jioni bado hatujamtambua.
Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Juma alisema kwamba iwapo tukio hilo litaachwa bila kufanyika kwa uchunguzi wa kumpata muhusika upo uwezekano mkubwa kwa wanawake kuendelea kutupa watoto.
Kwa upande wa Jeshi la polisi ,Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, amesema hana taarifa hizo, huku akiahidi kufutilia tukio hilo kwa ajili ya uchunguzi wa kina.

