Alhamisi , 24th Sep , 2020

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini, Dar es salaam, imeshindwa kutoa uamuzi katika kesi ya kugushi hati ya kiapo na kujipatia shilingi bilioni moja kwa njia ya udanganyifu, inayomkabili aliyewahi kuwa mgombea wa ubunge, Korogwe mjini kupitia Act-Wazalendo 2015 Salma Mtambo na mwenzake-

baada ya mshiakiwa wa pili kushindwa kufika mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliwakilishwa na mawakili Grace Mwanga na Wankyo Simon ambao  wamedai kuwa shauri hilo  lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kueleza kuwa mshtakiwa mmoja hajafika.

Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, amesema kuwa uamuzi wa shauri hilo uko tayari na kwamba hawezi kutoa uamuzi bila mshtakiwa wa pili ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea Mohammed Majaliwa, kuwepo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba mosi,2020.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano yakiwepo ya kugushi hati ya kiapo na kujipatia fedha za kitanzania shilingi bilioni moja kwa njia ya udanganyifu na kutotii amri halali ya Mahakama.