Rais Magufuli na Miraji Mtaturu
Mtaturu ameyabainisha hayo leo Septemba 17, 2019, ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais Magufuli alipompongeza na kuiagiza Wizara ya Maji, kuhakikisha inatatua changamoto na kero ya maji kupitia hoja aliyoiwasilisha Bungeni wakati akila kiapo siku ya Septemba 3, 2019.
''Kwahiyo nimefurahi namna ambavyo Mheshimiwa Rais amelipokea na kuelekeza Wizara ilifanyie kazi, kwahiyo mimi ntafuatilia ili kuhakikisha hiyo ahadi inatekelezwa na huduma inatolewa kwa wananchi'' amesema Mtaturu.
Aidha Mbunge Mtaturu ameongeza kuwa, licha ya uwepo wa changamoto hiyo kuzaa matunda kwa kuahidiwa itatuliwa kwa uharaka, amesema kuwa Septemba 20 anatarajia kurudi jimboni kwake na kukutana na wananchi na kuchapa kazi kama alivyowaahidi.
