Ijumaa , 10th Jul , 2020

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar aliyepitishwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Dkt Hussein Mwinyi, amesema kuwa licha ya kwamba katika maisha yake yote kufanya mitihani mingi, lakini amekiri kuwa mtihani mgumu na mkubwa ambao amepitia ni ule wa kuwania nafasi hiyo.

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi

Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai, 10, 2020, wakati akiwashukuru Wajumbe wote waliompigia kura, na kuongeza kuwa sasa hivi wanachama waache masuala ya utimu, badala yake wamuunge mkono na kuwa ni kitu kimoja na hata wale aliokuwa akishindana nao wameahidi kumuunga mkono.

"Hii ni heshima kubwa na kura nilizozipata ni nyingi sana na hii inaonyesha imani yenu juu yangu na mimi niwaahidi nitafanya kazi na kulitumika Taifa kwa nguvu zangu zote, na wenzangu wote wako tayari kushirikiana nami, sasa hivi hakuna timu Mwinyi wala nani sasa hivi tuna timu CCM, zoezi halikuwa rahisi, mimi katika maisha yangu nimefanya mitihani mingi lakini mkubwa kuliko wote ulikuwa ni huu, mkiona nimepungua pungua sababu ni hii" amesema Dkt Mwinyi.

Tazama video hii