Jumanne , 1st Dec , 2015

Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Jumanne Sagini amefanya ziara ya kushtukiza katika manispaa ya Dodoma kwa lengo la kujionea utendaji za umma zinavyoendeshwa na kutoridhishwa na kazi za watendaji katika idara zao.

Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Jumanne Sagini

Katika ziara hiyo amewataka watendaji na wakuu wa idara kuhakikisha kasoro zote alizokutana nazo katika halmashauri hiyo zinashughulikiwa haraka kabla hawajachyukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na sheria za utumishi.

Sagini alifanya ziara katika baadhi ya masoko ya halmashauri hiyo likiwemo soko la Sabasaba pamoja na machinjio ya kuku huku akionesha kutoridhishwa na hali ya usafi ya maeneo hayo na kutaka watendaji wawajibike.

Aidha Sagini alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku vilabu vya starehe ambavyo havijapewa vibali vya kupiga muziki kwa sauti ya juu mpaka usiku wa manane waache hivyo mara moja la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.