Jumatano , 8th Feb , 2017

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimeongezeka kutoka asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Desemba mwaka jana hadi asilimia 5. 2 ikiwa ni ishara kwamba kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma imeongezeka kwa wastani wa asilimia 0.2.

Ephraim Kwesigabo

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kutaja sababu ya ongezeko hilo kuwa ni kupanda kwa takribani bidhaa na huduma zote ambazo hutumika kupima mfumuko wa bei.

Kwa mujibu wa Bw. Kwesigabo, kasi ya mfumuko wa bei nchini ni ndogo ikilinganishwa na nchi za jirani za Uganda na Kenya na kwamba thamani ya shilingi mia moja katika manunuzi ya bidhaa na huduma imefikia shilingi 94 na senti 42 kutoka shilingi 95 na senti 20 ilivyokuwa mwezi Desemba.