Jumapili , 26th Feb , 2023

Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia leo ambapo watu waliovamia wamevunja mlango na kuingia ndani kisha kuharibu vitu vitakatifu vikiwemo mavazi ya misa na kuvunja misalaba.

Sehemu ya uharibifu uliofanywa

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlayi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na upepelezi wa tukio hilo unaendelea.

Taarifa zaidi kwa urefu itafuata.

Unaweza kutazama picha zaidi za tukio hilo hapo chini