watatu kushoto ni mwenyekiti wa Bodi Kampuni ya uwekezaji UTT
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa bodi Casmir Kyuki amesema pamoja na changamoto za covid 19 na mabadiliko ya sera ya uwekezaji katika nchi zinazoshirikiana na Tanzania bado utendaji wa soko umeendelea kuridhisha
''Kwa upande wa utendaji wa soko la mitaji na dhamana kumekuwa na mabadiliko madogo ya bei za hisa kwa kampuni za ndani Kama farhisi ya hisa za Tanzania zinavyoonyesha''amesema Casmir Kyuki
Sambamba na hilo Kampuni hiyo imezindua rasmi huduma ya usimamizi wa fedha UTT AMIS Wealth Management services yenye lengo la kuwekeza katika mifumo ya tehama ili kuwezesha wawekezaji waliowekeza kupata taarifa za Uwekezaji kwa njia ya simu kiganjani.