Jumapili , 28th Mei , 2023

Ikiwa leo Dunia inaadhimisha ni Siku ya Hedhi East Africa TV na East Africa Radio imezindua rasmi kampeni yake ya Namthamini yenye lengo la kumsaidia mtoto wa kike anayeishi katika mazingira magumu kupata taulo za kike zitakazomstiri kwa mwaka mzima.

Mabalozi wa kampeni ya #Namthamini Justine Kessy na Najma Paul

Uzinduzi wa kampeni hiyo msimu wa saba sasa umefanyika hii leo Mei 28, 20223, katika ofisi zake zilizopo Mikocheni Industrial Area jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa kampeni hiyo mmoja wa wadau waliojitokeza kuchangia kampeni hiyo amesema upo umuhimu wa Watanzania kuchangia kampeni hiyo kwani uhitaji wa taulo za kike kwa wasichana ni mkubwa kuliko ifikiriwavyo.

Kwa upande wao mabalozi wa kampeni hiyo Najma Paul na Justine Kessy, wamesema uwepo wa kampeni hiyo umekuwa na msaada mkubwa kwani kuna baadhi ya mikoa walikuwa wakifika baadhi ya wanafunzi hawazijui taulo za kike kabisa.