Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais amesema kuwa Tanzania itakua ni nchi pekee ambayo mwanafunzi wa kidato cha nne aliepata divisheni 4 akaingia chuo na kupewa mkopo wakati kuna wanafunzi wengine wamemaliza kidato cha sita hawapati mikopo.
Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa endapo suala hilo wangeendelea kulifumbia macho katika miaka ya mbele taifa lingetengeneza wasomi wasio na vigezo ambao wangeligharimu taifa katika uzalishaji.
Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake ambayo itakuwa ni ya viwanda lazima iwaajiri watu ambao wataleta ushindani katika uzalishaji sasa ikiwa hata watu walifeli wanaingia chuoni kwa ajili ya uzalishaji taifa litashindwa kufikia malengo yake.