Jumanne , 2nd Aug , 2016

Meneja uhusiano wakala wa usafiri wa haraka(DART) William Katambi amesema marekebisho ya mfumo wakutengeneza kadi maalum zakusafiria kwa magari ya mwendokasi UDART utakamilika baada ya siku mbili na watumiaji watazipata bila usumbufu.

Bwana Katambi ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Radio nakusema wanabadilisha mfumo huo kutokana na mfumo uliokuwepo haukua unakidhi viwango vya usafiri huo na idadi ya watumiaji wa usafiri wameongezeka.

Amesema wameanza mchakato mwingine wakupata mtu wakutengeneza kadi mpya takribani laki nane ambazo zitasaidia sana kupunguza uhaba wa kadi usitokee kwa siku za mbeleni na jukumu lamarekebisho yanafanywa na DART na mchakato wake utatumia mfumo wakutangaza tenda kwa wazabuni.

Amewataka wafanyakazi wa magari hayo kuwa waaminifu ili lengo la serikali la kuongeza pato la taifa litimie kutoka kwenye tozo mbalimbali zinazofanywa na DART na kuhakikisha wanatunza miundombinu yake.