Jumatatu , 20th Jun , 2016

Mradi wa mabasi yaendayo haraka umefanikiwa kuanza rasmi kutumia kadi za kielektroniki hii leo huku kukiwa na muitikio mkubwa wa watu katika kutumia kadi hizo.

Akiongea na East Africa radio Afisa habari wa mradi huo Bw Deus Bugaywa amesema kuwa waliandaa kadi laki mbili kwa kuanzia na mpaka kufikia mchana zaidi ya kadi elfu kumi zilikuwa zimeshachukuliwa.

Aidha nguvu kubwa ya ugawaji wa kadi hizo imeelekezwa maeneo ya Mbezi na Kimara kutokana na maeneo hayo kuwa na abiria wengi, Kuhusu suala la wanafunzi amesema kuwa wanaandaa utaratibu maalum ili waweze kuwapatia kadi zao lakini kwa hivi sasa hakuna kadi maalum kwa ajili ya wanafunzi.