Jumamosi , 27th Jul , 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemwagiza Afisa Elimu wa Wilaya ya Ruangwa anayeshughulikia Elimu ya msingi, Bw. Selemani Mrope, atafute walimu wawili kutoka Ruangwa na kuwahamishia kata ya Nanganga mara moja.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa maelekezo kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Ruangwa anayeshughulikia Elimu ya msingi, Bw. Selemani Mrope.

Ametoa agizo hilo leo mchana Jumamosi, Julai 27, 2019, wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nanganga, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, alipopita kuwasalimia wakazi hao.

"Lazima kuna walimu wamejazana pale Ruangwa mjini, leo tukitoka hapa nenda kaandike barua za uhamisho. Kesho Jumapili, wahusika wapewe barua zao na Jumatatu waje kuripoti hapa Nanganga," amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ambaye amewasili Lindi leo kwa mapumziko mafupi, alipokea taarifa ya shule ya msingi Nanganga ambayo ilionesha kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 237 ina walimu sita tu. Kati ya hao, wavulana ni 124 na wasichana ni 113.

Zaidi Tazama Video hapa chini