
Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda imeeleza kuwa taarifa hiyo ni uzushi na uchunguzi kwa waliosambaza unaendelea
“Taarifa hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo limelipwa tarehe 18 Agosti 2023, JWTZ inaujulisha Umma kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na upotoshaji kwa Jamii hivyo Watanzania waipuuze kwani ina nia ovu”
“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kufuatilia na kuchunguza kwa kina aliyehusika na upotoshaji huo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake”