Kocha huyo aliyetambulisha rasmi leo asubuhi majira ya Uingereza kuwa mrithi wa kocha Louis van Gaal, hakupoteza muda na kusema kuwa Manchester United ilipoteza muelekeo wake wa kutwaa mataji.
Jose Mourinho amesema anachotaka yeye ni kushinda Kombe la Ligi Kuu ya Uingereza, na kukataa kipimo cha yeye kuweza kufuzu kuingia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kama ndio mafanikio yake.
Pamoja na mambo mengine Mourinho amethibitisha kuwa mchezaji Henrikh Mkhitaryan ameshatia saini kujiunga na klabu hiyo na kubainisha kuwa kwa sasa wanawawania wachezaji wakubwa wanne huku nafasi kubwa akipewa Paul Pogba.








