Jumatano , 25th Jan , 2023

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo, amerithi kiti cha aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basilla Mwanukuzi.

Kushoto ni Jokate Mwegelo Mkuu mpya wa wilaya ya Korogwe, na kulia ni Basilla Mwanukuzi aliyeondolewa

Uhamisho wa Jokate kutolewa Temeke kupelekwa wilayani Korogwe mkoani Tanga, umefanywa hii leo Januari 25, 2023, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Ikumbukwe Basilla Mwanukuzi, amewahi kutwaa taji la ulimbende wa Tanzania (Miss Tanzania) mwaka 1998.

Hii leo Rais Samia ameteua wakuu wa wilaya wapya 37 huku 55 wakibaki kwenye wilaya zao na wengine 48 wamehamishwa wilaya. Idadi hiyo inafanya kuwa jumla yao kuwa wakuu wa wilaya 140 ambapo kati yao wanaume ni 100 na wanawake ni 40.