
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Charles Mlingwa, ambaye amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza vitendo vya ukosefu wa uaminifu kwa kampuni za ulinzi pamoja na kupunguza kuuawa kwa walinzi wasiokuwa na mafunzo yoyote.
Dkt. Mlingwa ameyasema hayo kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lidya Bupilipili katika hitimisho la mafunzo ya vijana zaidi ya 190 waliopitia mgambo na kupata mafunzo ya ulinzi kupitia JKT Kikosi cha Rwamkoma 822 KJ.
Mkuu wa Kikosi hicho, Luteni Kanali David Msakulo amesema vijana hao wameiva kufanya kazi za ulinzi katika kampuni mbalimbali kwa uaminifu huku mkurugenzi wa Suma JKT, Meja Alfred Mwaijande akiwataka kuepuka vitendo vya Rushwa.